MICHEZO

Ole Gunnar Solskjaer : “Pogba Anafa Kuwa Capteni”

on

Paul Pogba ana sifa za kuwa nahodha wa Manchester United, amesema kocha wa muda wa timu hiyo Ole Gunnar Solskjaer.Pogba alikuwa nahodha msaidizi wa United kabla ya kocha Jose Mourinho kumvua wadhifa huo mwanzoni mwa msimu.

Kiungo huyo mwenye miaka 25 alivaa kitambaa cha unahodha msimu huu katika mechi tatu wakati Antonio Valencia alipokuwa majeruhi. Hata hivyo alivuliwa madaraka hayo mwezi Spetemba.

“Namjua kijana huyu (Pogba) kwa muda sasa na ni kiongozi,” amesema Solskjaer, ambaye alimfunza Pogba akiwa kinda kati ya miaka ya 2008 na 2010.

“Ana ushawishi mkubwa mbele za watu. Anajali na uchu wa mafanikio.Maisha ya Pogba nje ya uwanja yamekuwa yakisimangwa sana, sawa na namna anavyotembea kwa madaha kabla ya kupiga mikwaju ya penalti msimu huu.

Lakini masimango hayo yanaonekana kugonga mwamba, na kiwango chake mchezoni kimeimarika maradufu toka Solskaer alipochukua mikoba ya Mourinho aliyetimuliwa kazi mwezi Disemba.

TOA MAONI YAKO HAPA

Leave a Reply