ELIMU

Sekondari Tumaini Lutheran Malinyi Yafutiwa Matokeo Ya Kidato Cha Nne 2018

on

Na,Jovine Sosthenes.
Baraza la Mitihani Tanzania (Necta) limefuta matokeo ya wanafunzi 57 wa kidato cha nne katika Shule ya Sekondari ya Tumaini Lutheran Seminari ya Malinyi mkoani Morogoro baada ya kubaini shule hiyo ilivujisha mtihani huo.
Mbali na kufuta matokeo hayo, Necta pia imekifungia kituo hicho kufanyika mtihani.
Hayo yameelezwa leo Alhamisi Januari 24 na Katibu Mkuu Mtendaji wa Baraza hilo, Dkt. Charles Msonde wakati akitangaza matokeo ya kidato cha nne kwa mwaka 2018 mkoani Dodoma.
Kufuatia hatua hiyo, Dkt. Msonde amesema wameagiza wahusika wote kuchukuliwa hatua wakiwemo polisi waliosimamia.
Aidha Necta pia imewafutia matokea watahiniwa 252 wa Kidato cha nne kutokana na udanganyifu, wakiwemo 71 wa kujitegemea na wawili walioandika matusi.
Katika Matokeo hayo, pia Necta imeitangaza Shule ya St. Francis ya MBEYA kuongoza katika matokeo hayo huku Shule ya Pwani Mchangani ya Unguja ikishika nafasi ya mwisho.
Necta pia imetangaza wanafunzi waliofanya vizuri zaidi kitaifa ambapo kwa wavulana nafasi hiyo imeshikwa na Hope Mwaibanje wa Shule ya Sekondari Ilboru ya Arusha huku kwa upande wa wasichana ikikaliwa kileleni na Maria Robert Manyama wa St. Francis ya Mbeya.
TOA MAONI YAKO HAPA

Leave a Reply