MICHEZO

Mbao FC Yaifanyia Maajabu Gor Mahia Yaitoa Nje Ya Michuano Ya SportPesa

on

Achana na habari za Mnyama Simba kufungwa bao 5 – 0 kutoka kwa AS Vita Club ya DR Congo au Bi Hindu kumfunda DiamondPlatnumz kuhusu kuoa. Kubwa kwenye mchezo wa soka hivi sasa ni michuano ya SportPesa inayoendelea uwanja wa taifa ambapo katika hali isiyo kuwa ya kawaida bingwa mtetezi timu ya Gor Mahia imeyaaga mashindano hayo baada ya kupokea kipigo kutoka kwa Mbao FC ya Tanzania.

Katika hali isiyokuwa ya kawaida na wala isiyotarajiwa na wengi mabingwa watetezi Gor Mahia wameyaaga mashindano hayo kwa kutolewa na timu changa ya Mbao FC kupitia mikwaju ya penati.Katika penati hizo Mbao FC imekosa moja kati ya tano ilizopiga wakati Gor Mahia wakikosa mbili kwenye mikwaju hiyo mitano.Mpaka dakika 90 zinakamilika timu hizo zilitoka sare ya bao 1 – 1 ghali iliyopelekea kupigwa mikwaju ya penati ili kupata mshindi atakayesonga hatua inayofuata.

Bao la kuongoza la Gor Mahia likifungwa na Denis Oliech kupitia mkwaju wa penati baada ya Amos Charles kuunawa mpira ndani ya 18 katika haraka za kuokoa wakati Mbao FC wakipata goli la kusawazisha kupitia Aboubakar Ngalema.

TOA MAONI YAKO HAPA

2 Comments

 1. IzettaBig

  January 28, 2019 at 10:28 pm

  Hi. Very interesting article but it’s hard to find robengo16.com in google.
  You are out of google’s top ten, so you can’t expect big traffic.
  You need high quality backlinks. And you can get them even for free, just search in google: wrastain’s tools

  • Robert Ngonya

   January 28, 2019 at 11:48 pm

   THANK YOU FOR VISITING US! WE ARE IN PROGRAMING FOR MAKE OUR BLOG TO BE NUMBER ONE ON SERACH ENGENE BELEAVE ME, ANDA WELCOME AGAIN

Leave a Reply