MICHEZO

Marcus Rashford Atimiza Michezo 150,Solskjaer Amlinganisha Na Magwiji Wa UNITED

on

Muda mchache baada ya kushinda mechi yake ya saba na kuzidi kujiwekea rekodi akiwa meneja mpya ndani ya klabu ya Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer amwagia sifa nyota wake Marcus Rashford.

Solskjaer amesema kuwa kiwango anachokionyesha Rashford ni kipimo tosha cha nyota huyo kujiamini na kumlinganisha kipaji chake na lejendi Wayne Rooney na mchezaji bora kabisa duniani Cristiano Ronaldo.

‘’Kama utaangalia mwanzo wake, niliwaambia kwamba ni mchezaji mdogo zaidi ya Ronaldo na Rooney kufikisha jumla ya michezo 150 akiwa ndani ya Manchester United,’’ amesema Solskjaer.

‘’Sio mbaya, amefikisha michezo 150 akiwa na umri wa miaka 21, lakini pia uwezo wake umekuwa mkubwa na amekuwa mzuri kwenye safu ya umaliziaji na ni ndoto zangu kuwa na mchezaji kama yeye kwenye timu,’’

Alipoulizwa kama Rashford anaweza kumuweka kwenye kariba ya Rooney na Ronaldo walivyokuwa United wakati wa zama hizo bila kusita Solkjaer alisema ndiyo anamuweka kwenye levo hizo za juu kabisa.

TOA MAONI YAKO HAPA

Leave a Reply