BUNGENI

Halima Mdee Atinga Bungen ,Kamati Ya Shindwa Kusema Neno

on

Mbunge wa Kawe Halima Mdee alifika mbele ya Kamati ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge ikiwa ni kutekeleza agizo lililotolewa na Spika Job Ndugai ya kumtaka ahojiwe kuhusu tuhuma za kuunga mkono kauli ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG) Prof. Mussa Assad kwamba Bunge ni dhaifu.Mdee aliyeongozana na rafiki yake ambaye ni Mbunge wa Bunde Mjini Ester Bulaya aliwasili katika viwanja vya Bunge mnano saa 5 za asubuhi ambapo alianza kuhojiwa na kamati hiyo hadi majira ya saa 7 za mchana.

Mara baada ya mahojiano kumalizika Mwenyekiti wa Kamati hiyo Emmanuel Mwakasaka hakuweza kuzungumza na Waandishi wa habari kama ilivyo kawaida ya kueleza kilichojiri kwa madai kwamba hana nafasi.

TOA MAONI YAKO HAPA

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *