HABARI ZA MASTAR

Chris Brown Ashikiliwa Na Polisi Ufaransa Kisa Tuhuma Za Ubakaji

on

Kwa mujibu wa mtandao wa Reuters unaripoti kuwa mwimbaji wa RnB Chris Brownanashikiliwa na polisi nchini Ufaransa kwa uchunguzi dhidi ya tuhuma za ubakaji.

Inaripotiwa kuwa Chris Brown atapanda kizimbani siku kadhaa zijazo baada ya mwanamke mmoja kumburuza Breezy Mahakamani baada ya kudai kuwa aliwahi kubakwa mnamo January 15- 16 mwaka 2019 walipokuwa nchini Ufaransa kwenye hoteli ya Le Mandarin Oriental.

Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 24 anadai kuwa Chris Brown alimualika chumbani kwake katika hoteli hiyo kwa nia ya mazunguzmo lakini mwisho wa siku aliishia kumbaka.

 

TOA MAONI YAKO HAPA

Leave a Reply