KIMATAIFA

Kupatwa Kwa Mwezi Gafla

on

Wachunguzi wa anga wamekuwa wakitafuta tukio lisilo la kawaida la kupatwa kwa mwezi ambalo lilianza siku ya Jumapili usiku.

Wakati wa tukio hilo mwezi huo unaojulikana kama ‘Super Blood Moon’, hubadilika na kuwa mwekundu , huku ukionekana kuwa na mwangaza mwingi na ulio karibu na dunia zaidi ya ilivyo siku za kawaida

Tukio hilo lilikuwa likionekana kutoka Kaskazini na marekani kusini, pamoja na magharibi mwa Ulaya. Nchini Uingereza, mawingu mengine yalizuia kuonekana kwa mwezi huo vizuri.

Kupatwa kwa mwezi kunatarajiwa katika kipindi cha miaka miwili, mnamo tarehe 26 mwezi Mei 2021

Walter freeman , naibu profesa katika chuo kikuu cha Syracuse University mjini New York state, alisema: “mwanga mdogo wa jua hutolewa na dunia na kufika katika mwezi, ukijipinda kando kando ya dunia.

Kiwango hiki cha rangi nyekundu huangazia mwezi vya kutosha kwa binadamu kuweza kuona.

Tukio hili hujiri wakati dunia inapopita katikati ya Jua na mwezi.

Katika hali hii, jua huwa nyuma ya dunia huku mwezi ukizunguka katika kivuli cha dunia.

Kupatwa kwa mwezi kulianza mwendo wa 02:35 GMT siku ya Monday na kukamilika saa 07:49 GMT, lakini kipindi ambacho mwezi wote ulikuwa mwekundu ilikuwa mwendo wa 05:12 GMT.

Tukio hilo lisili la kawaida hupata jina ‘Super’ kutokana na swala kwamba mwezi utakuwa karibu mno na dunia- ambapo utaonekana mkubwa angani zaidi ya ilivyo kawaida.

Nalo Jina “wolf” linatokana na majina yanayopewa miezi mikubwa mwezi Januari “wolf moons”.

 

TOA MAONI YAKO HAPA

Leave a Reply