KITAIFA

WAZIRI MPINA AIBUA UFISADI MKUBWA KWENYE BIASHARA YA CHANJO +VIDEO

on

WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina ameibua ufisadi wa kutisha katika biashara ya chanjo za mifugo na kumuagiza Mkurugenzi wa Huduma za Mifugo nchini (DVS) kuandaa haraka mwongozo utakaosimamia mfumo mzima wa uzalishaji, uagizaji, usambazaji na uchanjaji wa mifugo na kuweka bei elekezi itakayowezesha wafugaji kupata chanjo kwa gharama nafuu.

Mpina amesema kwa miaka mingi wafugaji wamefanyiwa dhuluma kubwa kwa kuuziwa chanjo zaidi ya mara tano ya bei halisi licha ya baadhi ya chanjo hizo kuzalishwa na Taasisi ya Chanjo za Mifugo Kibaha (TVI) ambayo ni Taasisi ya Serikali iliyopewa jukumu la kurahisisha upatikanaji wa chanjo na kwa gharama nafuu.

Waziri Mpina amesema Taifa limefikia hapo kutokana na kukosekana usimamizi madhubuti wa utoaji chanjo nchini hali iliyochangia kuwakatisha tamaa wananchi kuhudumia mifugo yao na kusababisha mingi kufa kwa kukosa chanjo ambapo amesisitiza kuwa Serikali ya awamu tano inayoongozwa na Dk John Pombe Magufuli haitakubali dhuluma hiyo iendelee tena.

Akizungumza mara baada ya kutembelea Taasisi ya Chanjo Kibaha (TVI) na Wakala wa Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA), Waziri Mpina ameelezea kusikitishwa kwake na usimamizi dhaifu wa mfumo wa ununuzi, usambazaji na uchanjaji wa mifugo nchini na kutaka hatua za haraka zichukuliwe ili kuondoa dosari hizo.

EXTR NEWS:WAZIRI MPINA AIBUA UFISADI MKUBWA BIASHARA YA CHANJO::

TOA MAONI YAKO HAPA

Leave a Reply