MICHEZO

SADNEWS:Mmiliki Wa Klabu Ya Leicester City Afariki Dunia

on

Klabu ya Leicester City ya nchini Uingereza imetangaza kuwa mmiliki wa klabu hiyo raia wa Thailand, Vichai Srivaddhanaprabha amefariki dunia katika ajali ya helikopta nje ya uwanja wa klabu hiyo, King Power.

 Bosi huyo ambaye pia ni Mwenyekiti wa klabu hiyo alikuwa ni mmoja kati ya watu watano waliopoteza maisha katika ndege hiyo, ajali iliyotokea Jumamosi ya wiki iliyopita.

Ndege hiyo ilitua katika eneo la kuegesha magari karibu na uwanja, muda mfupi baada ya kuruka, mara bada ya kumalizika kwa mchezo wa Leicester City na West Ham United, mchezo ambao timu hizo zilitoka sare ya bao 1-1.

Taarifa rasmi ya Leicester City, imesema: “Katika hali ya kuhuzunisha na kuumiza, tunathibitisha kwamba Mwenyekiti wetu, Vichai Srivaddhanaprabha alikuwa ni mmoja ya watu waliopoteza maisha katika Jumamosi jioni baada ya helicopta iliyombeba pamoja na watu wengine wanne kuanguka nje ya uwanja wa King Power“.

ADD YOUR COMMENTS

TUACHIE MAONI YAKO HAPA