KIMATAIFA

13 Wafariki Katika Makabiliano Ya Kundi La Wapiganaji Nchini Kamerun

on

Watu 13 waripotiwa kufariki  katika makabiliano kati ya jeshi la kundi la wapiganaji wanaotaka kujitenga nchini Kamerun.

Wanamgambo  hao wanaotaka kujitenga wanatokea upande  unaozungumza lugha ya kiingereza nchini Kamerun.

Miongoni mwa watu waliofariki  wamo raia watatu ambae wamefariki kwa kupigwa risasi.

Wanajeshi wawili na wanagambo wanene pia wamefariki katika makabiliano hayo yaliozuka upya Jumanne.

Makabiliano hayo yamezuka Kusini-Magharibi mwa Kamerun  muda mchache baada ya kutangazwa matokeo ya uchaguzi na kumtangaza Paul Biya mshindi katika uchaguzi huo uliofanyika nchini Kamerun kwa kupata asilimia 71,2 ya kura.

ADD YOUR COMMENTS