KIMATAIFA

Watoto Wa Mwanahabari Aliye uawa “Jamal Khashoggi”Wapokelewa Katika Karsi Ya Mfalme Saudia

on

Watoto wa mwanahabari  alieuawa katika ubalozi mdogo wa Saudia wapokelewa katika karsi ya mfalme Saudia

Mfamle wa Saudia na mwanamfalme wawapokea watoto wawili wa mwanahabari  Jamal Khashoggi alieuawa  Istanbul katika karsi ya mfalme

Mfalme wa Saudia Salman Bin Abdulaziz na Mohammed Bin Salman wawapokea watoto wawili wa Jamal Khashoggi  Jumanne katika karsi ya mfalme. Ifahamike kuwa utawala wa Saudia wakiri kuuawa kwa Jamal Khashoggi  baada ya kukana kwa muda wa zaidi ya siku 15.

Jamal Khashoggi alionekana kwa mara ya mwisho  akiingia katika ubalozi mdogo wa Saudia mjini Istanbul Oktoba 2.

Sahl na Salah  ndio majina ya watoto wa Jamal Khashoggi waliopokelewa katika karsi ya mfalme al Yamama mjini Riyadh. Taarifa hiyo imetolewa na jarida la SPA.

Mfalme wa Saudia  na mwanamfalme  wametoa salamu za rambirambi kwa familia ya Jamal Khashoggi. Jarida hilo limefahamisha kuwa watoto  hao wa Khashoggi wamepokea salamu hizo na kutoa shukrani kwa ushirikiano  baada kufuatia kifo cha baba yao.

Rais wa Uturuki Recep Tayyıp Erdoğan amefahamisha katika hotuba yake kuwa  ni dhahiri kuwa Jamal Khashoggi aliuawa na kifo chake kilipangwa.

ADD YOUR COMMENTS