KITAIFA

VIDEO:Wanafamilia Wauawa Na Kutupwa Mtoni Mkoani Songwe

on

Ni muda sasa tangu kusikika kwa matukio ya mauaji katika Mkoa mpya wa Songwe Wilayani Mbozi, lakini leo september18 2017 kumetokea tukio la kushangaza tena katika maeneo ya daraja la Mlowo lililopo katika barabara ya kutoka Tunduma kwenda Mbeya.

Watu watatu wakiwamo mume na mke wake, wakazi wa Mji mdogo wa Mlowo wilayani Mbozi Mkoa wa Songwe wamekutwa wameuawa na kisha miili yao kutupwa chini ya daraja la Mto Mlowo. Waliofariki ni Luka Humri, Bahati Mohamed na mwingine ametambulika kwa jina maarufu la Mama Dina.

Maiti hizo ziliondolewa na jeshi la polisi kwa uangalizi wa Mkuu wa mkoa wa Songwe Nicodemas Mwangela. Nicodemas Mwangela amesema tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo  Septemba 7, 2018 na mtu wa tatu ni jirani wa mume na mke waliouawa.

Alisema wauaji hao baada ya kutekeleza tukio hilo wamewachukua kisha kwenda kuwatupa kwenye daraja la mto huo.

Mwangela amewaomba wakazi wa Mlowo kuwa watulivu wakati jeshi la Polisi likiendelea na uchunguzi wa tukio hilo.

“Niwaombe sana ndugu zangu hebu kuweni watulivu kutokana na tukio hilo baya kabisa. Lakini wakati vyombo vya ulinzi na usalama vikiendelea na uchunguzi wa kiini juu ya watu hawa kuawa, niwaombe tena toeni ushirikiano kwa vyombo hivi kwa yoyote kutoa taarifa zinazohitaji ili kuwabaini waliotekeleza mauaji haya,” amesema.

Kamanda wa polisi mkoa wa Songwe Mhe. Nyage amethibitisha kutokea kwa tukio hilo kuwa miili iliyookotwa ni ya mwanaume mmoja na wanawake wawili katika daraja la Mlowo.

Mathias Nyange amesema wanandoa hao walikuwa wafanyabiashara katika Soko la Sokowo  na chanzo cha mauaji hayo bado hakijafahamika lakini upelelezi umeanza ikiwa ni pamoja kuwatambua kwa majina marehemu hao.

Juhudi za kuwatafuta ndugu wa marehemu ziliendelea ingawa baadhi yao walikuwa kati mahojiano na jeshi la polisi ili kuua nini chanzo cha mauaji hayo ambayo hadi hivi sasa chanzo chake hakijafahamika.

Wananchi na wakazi wa mlowo wameonekana kujawa na hofu na kuwa na simanzi juu ya tukio hilo huku wakilaani kuwa linaharibu sifa ya mkoa wao, ilihali kuwa Songwe ni Mkoa safi na salama.Mkazi mmoja wa Mlowo, Joseph Mwashiuya amesema tukio hilo limewashtua na kuufanya mji  kutikisika kwani sio la kawaida na kuiomba Serikali kuimarisha ulinzi wakati huu.

VIDEO:BONYEZA PLAY BATANI KUTAZAMA TUKIO LA MAUAJI YALIYOTOKEA MKOANI SONGWE -MLOWO

ADD YOUR COMMENTS