BURUDANI

Tiwa Savage Ashindwa Kutolewa Hotelini Nchini Kenya Kwa Kushindwa Kulipa Bajeti…Ilikuaje Hii Hapa Full Stori

on

Mwanamuziki nyota mwenye asili ya Nigeria Tiwa Savage amelalamika na kudai aliachwa hotelini bila gharama kamili ya malazi kulipiwa kama yalivyokuwa maafikiano katika ziara yake nchini Kenya.

Savage, 38, amelalamika kwamba pia alikosa gari la kumsafirisha kwenda uwanja wa ndege kama ilivyokuwa matarajio.

Anaonekana kugundua kwamba bili ya malazi haikuwa imelipiwa yote wakati wa kuondoka hotelini. Hata hivyo, hajaeleza alikuwa amelala katika hoteli gani.

Savage, ambaye jina lake kamili ni Tiwatope Savage-Balogun, alikuwa amezuru Kenya kutumbuiza katika hafla ya uzinduzi wa almabu mpya ya mwanamuziki nyota kutoka Kenya kwa jina Redsan siku ya Jumamosi. Mwanamuziki wa Jamaica Demarco pia alitumbuiza.

Uzinduzi wa albamu hiyo kwa jina Baddest ulifanyika katika mghahawa maarufu wa Carnivore, na hafla hiyo ilitangazwa sana kwenye mitandao na vyombo vya habari. Savage amesema alijaribu kumpigia simu promota aliyekuwa amemwalika kuja Kenya bila mafanikio.

Aliwatetea wasanii akisema hawawezi kulaumiwa kwa kulalamika kila mara kuhusu mapromota, iwapo matukio kama hayo yatafanyika.

Ameandika hata hivyo kwamba bado anaipenda Kenya na ataendelea kutumbuiza mashabiki wake.

Baadhi ya Wakenya wameonekana kukerwa na tukio hilo na kuliona kuwa la aibu.

@RonoKech ameandika: “Hawajefanyia Tiwa Savage poa.”

@Ms_Arim ameandika kwamba ‘mwanamuziki huyo anafaa kuwataja hadharani na kuwaaibisha wote waliohusika’.

Wengine hata hivyo wamemtania mwanamuziki huyo.

Kwa mfano @iNaheemMUFC ambaye ameandika: “Tiwa Savage anafaa kujua pesa tuliomba wachina loan tulinunua nazo uniform mpya za makarao hatTiwa Savage anafaa kujua pesa tuliomba wachina loan tulinunua nazo uniform mpya za makarao hata promoters pia hawana kakitu. Tumesota.”

Anatania kwamba Wakenya wameishiwa na pesa pekee walizokopa zilitumiwa kununua sare mpya za polisi.

ADD YOUR COMMENTS