MICHEZO

Tetesi Za Soka Barani Ulaya Leo September 11

on

Kiungo wa kati wa Arsenal Mjerumani Mesut Ozil, 29, anawindwa na klabu ya Uturuki ya Fenerbahce. (Fotomac)

Tottenham wanamfuatilia beki wa Leicester City mwenye miaka 21 Ben Chilwell, ambaye ameitwa kwenye kisosi cha England na ambaye amepangwa kwa ofa ya mchezaji wa Ajax raia wa uholanzi Frenkie de Jong, 21. (Telegraph)

Mshindi mara nne wa Ligi ya Premio Edwin van der Sar, 47, amesema hajiungi katika kikosi cha kiufundi huko Manchester United.(Sky Sports)

Chelsea ililipa zaidi kwa karibu pauni milioni 40 wakati ilitumia pauni milioni 7 kwa kipa wa Athletic Bilbao mwenye miaka 23 Kepa Arrizabalaga mwezi Agosti kwa mujibu wa shirika la uanngalizi wa kandanda CIES. (Football Italia)

Kiungo wa kati wa Charlton Athletic mwenye miaka 16 Jeremy Sarmiento, ambaye alizaliwa huko Madrid kwa wazazi kutoka Ecuador anakaribia kujiunga na klabu ya Ureno ya Benfica licha ya Manchester City kumwinda. (London Evening Standard)

Mlinzi wa Manchester United Luke Shaw, 23, huenda akakosa mechi mbili ya klabu chake baada ya kupata jheraha akiichezea England. United watacheza na Watford siku ya Jumapili kabla ya kusafiri kwenda Uswizi kukutana na Young Boys kwenye ligi ya mabingwa Jumatano ijayo. (Mirror)

West Bromwich Albion hawawezi kumpoteza mshambuliaji Dwight Gayle, 28, msimu huu licha ya ripoti kuwa vilabu vya China vinanammezea mate mshambuliaji huyo. Gayle yuko kwenye mkopo wa msimu wote kutoka Newcastle United. (Express & Star)

Fainali ya ligi ya mabingwa itaandaliwa mjini New York siku za usoni, kwa mujibu wa mfanyabiashara mmoja. Kuanzia mwaka 2021 na kuendelea, hakuna maeneo yaliyoathiriwa kwa fainali hizo. (Sun)

Klabu ya Derby County imepewa zaidi ya viti 8,500 kwa mechi ya kombe la Carabao huko Manchester United tarehe 25 mwezi Septemba. (Derby Telegraph)

Kiungo wa zamani wa kati wa Aston Villa Khalid Abdo, 21, amerudi nyumbani Sweden kufanya mazoezi na klabu ya huko Stockholm AIK. (Birmingham Mail)

Ofa za Tottenham na Barcelona zimekataliwa kwa kiungo wa kati wa Ajax mwenye miaka 21 Frenkie de Jong. (Mundo Deportivo – in Spanish).

Beki wa Manchester United wa miaka 23 raia wa England Luke Shaw anasababisha klabu yake kungoja kuhusu mkataba wake mpya, Mkataba wake wa sasa unakamilika mwishoni wa msimu.

Kiungo wa kati wa Ufaransa na Manchester United Paul Pogba 25, anasema kumekuwa na vitu vidogo kati yake na Jose Mourinho lakini uhusiano wao ni ule ule. (TF1, via Express)

Gareth Southgate atafanya mabadiliko tisa kwa kikosi chake cha England kwa mechi ya siku ya Jumanne na Uswizi. (Mirror)

Vilabu vya ligi ya Premio vitakubaliana kuhusu tarehe ya misho ya kununua wachezaji iwe Agosti 31. (Sun)

Kiungo wa kati wa Real Madrid mwenye miaka 32 Sergio Ramos anasema alipokea vitisho vya kuuawa kufuatia kuhusika kwake wa jeraha la mshambulizi wa Liverpool raia wa Misri Mohamed Salah, 26, wakati wa fainali ya ligi ya mabingwa mwezi Mei. (ESPN)

Meneja wa Real Madrid Zinedine Zidane anasema anata kurudi kwenye usimamizi hivi karibuni. (RTVE, via Marca). Roma wanataka kumsani kiungo wa kati wa Porto mwenye miaka 28 Hector Herrera. (Corriere dello Sport – in Italian)

ADD YOUR COMMENTS