MICHEZO

Golikipa Wa Tottenham Hotspurs “Hugo Lloris” Mikononi Mwa Polisi Jijini London

on

Golikipa wa timu ya taifa ya Ufaransa anayeichezea club ya Tottenham Hotspurs ya England Hugo Lloris, leo August 24 2018 amerudi kwenye headlines baada ya kukamatwa na Polisi jijini London.

Hugo Lloris ambaye alikuwa sehemu ya kikosi cha Ufaransa kilichotwaa Kombe la Dunia 2018 nchini Urusi, amekamatwa na kuwekwa mahabusu kwa saa saba baada ya kugundulika kuwa alikuwa akiendesha gari huku akiwa kalewa.

Metropolitan Police wamethibitisha kuwa staa huyo kwa sasa yupo nje kwa dhamana na atalazimika kwenda Mahakamani September 11 2018 kuhusiana na kesi hiyo, Tottenham sasa inajiandaa na mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Man United Jumatatu ya August 27.

ADD YOUR COMMENTS