BannerFans.com

BURUDANI

Snoop Dogg aikubali ngoma ya Ycee kutokea Nigeria

on

Staa wa muziki kutokea Nigeria Ycee ambaye anatamba na ngoma yake ya “Say Bye Bye” anazidi kuipeleka midundo ya Kiafrika kimataifa na hii ni baada ya staa mkongwe wa Hip Hop Marekani Snoop dogg kukubali ngoma yake ya “Juice” aliyomshirikisha Maleek Berry.

Kupitia instagram account ya Ycee amepost kipande cha video cha Snoop Dogg akisikiliza ngoma hiyo ya “Juice” na kuandika “Kitu kinachohitajika sana ni tabasamu kwenye uso wangu ninapotazama video hii”

Ycee aliachia ngoma hiyo ya Juice April 8,2017 akiwa kamshirikisha mkali mwenzake kutokea Nigeria Maleek Berry na mpaka sasa ngoma hiyo ina views Millioni 21.

ADD YOUR COMMENTS

You must be logged in to post a comment Login