Askari Wa Jeshi JKT 10 Wafariki Katika Ajali Ya Basi Mkoani Mbeya - OFFICIAL ROBENGO BLOG
BannerFans.com

KITAIFA

Askari Wa Jeshi JKT 10 Wafariki Katika Ajali Ya Basi Mkoani Mbeya

on

Basi lenye namba za usajili T 755 BAB lililokuwa likisafiri kutoka mkoani Tabora kuelekea mkoani Mbeya, limepata ajali leo Alhamisi, Juni 14, 2018 katika eneo la Igodima jijini Mbeya na kusababisha vifo vya askari 10 wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) waliokuwa wakitoka mafunzoni na kujeruhi wengine kadhaa.
Taarifa za awali kutoka eneo la tukio zinadai kuwa, basi lililokuwa limewabeba wanajeshi wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania lililokuwa likitokea Tabora kuelekea Mbeya limepinduka katika mteremko wa Igodima, Mbeya.
Chanzo cha ajali hiyo kimesekana kuwa ni mwendokasi uliopelekea  kukatika kwa ‘break’ kutokana na mteremko mkali katika eneo la Igodima na kuangukia korongoni.

ADD YOUR COMMENTS

You must be logged in to post a comment Login