KIMATAIFA

G7:Kuchangia dola bilioni 3 kwa ajili ya elimu ya wasichana

on

Canada imesema ina mipango ya kuchangia kiasi cha pauni bilioni 2.9 ikisaidiwa na nchi washirika wa G7 kwa ajili ya kusaidia elimu ya wasichana na wanawake walio masikini

Fedha hizo zitasaidia kuhakikisha kuwa mpango wa wasichana na wanawake kupata elimu sawa na wavulana na kuwezesha fursa za kujifunza katika nchi mbalimbali duniani, Serikali ya nchi hiyo imeeleza.

Tangazo hili la siku ya Jumamosi limekuja kwa kuchelewa kwa kuwa nchi washirika wakiwemo Ujerumani,Japan, Uingereza, Umoja wa Ulaya na Benki ya dunia zilikuwa zikiendelea kuchangia

Mkutano wa G7 uliofanyika Quebec ni mkutano wa mwaka unaokutanisha nchi za Canada, Marekani, Uingereza, Ufaransa, Italia, Japan na Ujerumani.

Changamoto ya elimu inayowakabili wasichana duniani

Serikali ya Canada imesema kujitoa kwa ajili ya kuchangia elimu kunawakilisha ”uwekezaji mmoja mkubwa katika elimu kwa ajili ya wanawake na wasichana wanaokuwa katika mazingira yenye changamoto kadha wa kadha”.

Uwekezaji huu unaelezwa kuwa utaweza kuwasaidia watoto na vijana wadogo zaidi ya milioni nane.

Mshindi wa tuzo ya amani ya Nobel Malala Yousafzai, 20 ameunga mkono zoezi hilo la uchangaji fedha.

Inakadiriwa kuwa watoto milioni 75, wengi wao wasichana, wameacha shule katika nchi 35 zilizokabiliwa na mizozo duniani, kwa mujibu wa shirika la umoja wa mataifa linalohudumia watoto, Unicef.

Uingereza ni miongoni mwa nchi zilizotoa mchango mkubwa.Imesema itawekeza dola milioni 250, na Benki ya dunia itachangia dola bilioni 2 kwa kipindi cha miaka mitano.

Canada ilisema itachanga dola milioni 310 kwa kipindi cha miaka mitatu .

Kwa mujibu wa taarifa ya nchi hiyo, uwekezaji huo utasaidia mambo haya:

  • Kuwawezesha wanawake na wasichana kupata ujuzi unaohitajika kwa ajili ya ajira
  • Kuboresha mafunzo kwa waalimu ili kuweza kutengeneza mitaala bora kwa ajili ya wanawake na wasichana.
  • Kusaidia uvumbuzi wa njia za utoaji elimu, hasa kwa jamii ambazo ni ngumu kuzifikia zikiwemo zilizokimbia makazi na wakimbizi.
  • Kusaidia nchi zinazoendelea katika jitihada za kuwapatia fursa sawa wasichana kumaliza angalau miaka 12 ya kupata elimu bora, kutoka shule za msingi mpaka sekondari.

ADD YOUR COMMENTS

You must be logged in to post a comment Login