Licha Ya Kukosa Ubingwa Wa UEFA Liverpool Yamsajiri Fabinho Henrique Tavares - OFFICIAL ROBENGO BLOG
BannerFans.com

MICHEZO

Licha Ya Kukosa Ubingwa Wa UEFA Liverpool Yamsajiri Fabinho Henrique Tavares

on

Liverpool imekubali kumsajili kiungo wa Monaco Fabio Henrique Tavares maarufu kama Fabinho kwa ada ya Paundi Milioni 40 ambayo inaweza kuongezeka kutokana na kiwango cha mchezaji.

Fabinho mchezaji wa kimataifa wa Brazil mwenye miaka 24 atajiunga na Liverpool Julai 1.

Kiasi cha ziada cha ada ya uhamisho wake ambacho ni Paundi Milioni 5 kinaweza kuongezeka kutokana na mafanikio atayoipa Liverpool.

Kuwasili kwake ni kwa ajili pia ya kuziba pengo la Emre Can ambaye anatarajiwa kutimkia kwa mabingwa wa Seria A Juventus muda wowote.

”Hiki ni kitu ambacho sikuzote nimekuwa nikikitamani- hii ni timu kubwa, ”alisema Fabinho. ”Nimefurahishwa sana.”

Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp amesema ”Huyu ni mchezaji ambaye ana faida sana uwanjani, anaweza kucheza nafasi nyingi, namba sita, nane ama namba mbili’. Hili ni jambo zuri sana.”

Fabinho ambaye mkataba wake unatarajiwa kuanza Julai 1 amesema Liverpool ni klabu yenye miundombinu mizuri na ya kuvutia.

ADD YOUR COMMENTS

You must be logged in to post a comment Login