Maneno Ya Pep Guardiola Kwa Tuhuma Za Yaya Toure - OFFICIAL ROBENGO BLOG
BannerFans.com

MICHEZO

Maneno Ya Pep Guardiola Kwa Tuhuma Za Yaya Toure

on

Ikiwa imesalia siku moja kabla ya club ya Man City inayofundishwa na kocha Pep Guardiola imuage rasmi kiungo wake raia wa Ivory Coast Yaya Toure leo kocha wao Pep Guardiola ameongea na waandishi wa habari.

Pep Guardiola amelazimika kuzungumza mambo kadhaa kuhusiana na Yaya Toureikiwemo swali kuhusu Yaya Toure kama bado anaona anaweza kuendelea kucheza EPLkatika club nyingine yoyote kitu ambacho Guardiola alikiri kuwa ndio.

“Wachezaji ndio wanafanya club kuwa kubwa Toure ameisaidia club kupiga hatua natumaini tutacheza mchezo mzuri kesho tutacheza kwa ajili ya Toure, sitamuhukumu Toure kwa kiwango chake alichokionesha msimu huu, labda inawezekana nikawa nilikosea katika maamuzi yangu lakini sijui”>>>  Guardiola 

“Toure anapenda kucheza niliyachukua maamuzi haya tulipokuwa kwenye uwanja wa mazoezi naamini ataendelea kucheza vizuri na kurudi  inawezekana Man City au sehemu nyingine yoyote bado ana hamu ya kucheza na ushauri wangu kwake ni kuendelea kucheza”>>>Guardiola

Yaya Toure kesho ndio atacheza game yake ya mwisho akiwa na Man City katika uwanja wa Etihad dhidi ya Brighton, hata hivyo msimu huu haukuwa mzuri kwake kwani ameanza katika game 16 pekee na kati ya hizo game nne za Carabao Cup.

ADD YOUR COMMENTS

You must be logged in to post a comment Login