Real Madrid Watwaa Taji La UEFA 2018, Sarah Kukosa Kombe La Dunia 2018! - OFFICIAL ROBENGO BLOG
BannerFans.com

MICHEZO

Real Madrid Watwaa Taji La UEFA 2018, Sarah Kukosa Kombe La Dunia 2018!

on

KYIV: Klabu ya soka ya Real Madrid imefanikiwa kuchukua kombe la UEFA Champions League, #UCL kwa mara ya 3 mfululizo baada ya kuifunga Liverpool goli 3-1

Kocha wa Real Madrid, Zinedine Zidane anakuwa kocha wa kwanza kushinda kombe hilo mara tatu mfulizo huku Mchezaji Gareth Bale akiwa mchezaji wa kwanza kutoka benchi na kufunga magoli mawili.

Mchezaji wa Soka wa Liverpool na Raia wa Misri, Mohammed Salah ameumia bega na kuna uwezekano akakosa kucheza katika Michuano ya Kombe la Dunia 2018.

Kwa mujibu wa Shirika la Utangazaji la BBC, Salah ameteguka bega hivyo anaweza kukosa kushiriki Kombe la Dunia la mwaka huu.

Inasemekana mtu aliyeteguka bega anachukua wiki 12 hadi 16 kupona kabisa. Kwa mfano, mchezaji Jamie Carragher aliyekuwa anachezea timu ya Liverpool alipata tatizo kama hilo katika msimu wa 2010/11 na alikaa nje kwa miezi miwili.

ADD YOUR COMMENTS

You must be logged in to post a comment Login