TANZIA :Mkuu Wa Mkoa Mstaafu Abas Kandoro Aaga Dunia - OFFICIAL ROBENGO BLOG
BannerFans.com

KITAIFA

TANZIA :Mkuu Wa Mkoa Mstaafu Abas Kandoro Aaga Dunia

on

TANZIA: Aliyewahi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Abbas Kandoro amefariki dunia usiku huu wa Ijumaa, Aprili 27, 2018 katika Hospitali ya Taifa, Muhimbili alikokuwa amelazwa akipatiwa matibu.

Kabla ya hapo, Kandoro alikuwa amelazwa katika Hospitali ya Benjamin Mkapa jijini Dodoma. Kabla ya kustaafu utumishi wake, Kandoro alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya kabla ya kumwachia Amos Makalla.

Aidha, Abbas Kandoro aliwahi kushika nafasi ya ukuu wa mikoa katika zaidi ya mikoa sita Tanzania Bara ikiwemo Dar es salaam, Mwanza, Arusha, Singida na Mbeya. Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda ameandika “Hata nakosa maneno ya kusema, Nakumbuka mwaka 2010 ulipokuwa Rc Mwanza namna ulivyosaidia katika Mgogoro wa kidini. Mungu akupe pumziko la milele mzee wangu”

ADD YOUR COMMENTS

You must be logged in to post a comment Login