KIMATAIFA

Mtendaji Mkuu wa Mtandao wa Kijamii Facebook Aomba Radhi

on

Mtendaji mkuu wa mtandao wa kijamii Facebook, Mark Zuckerberg ameomba msamaha kwa kamati ya Seneti ya Marekani kwa kuruhusu makampuni kadhaa kutumia vibaya data binafsi za jukwaa hilo kisiasa.

Kinyume na matarajio ya ulimwengu, wakati wa utetezi Mark badala ya kuvaa fulana kama alivyozoeleka, alikuwa maevalia nadhifu suti nyeusi, Mark amesema kwamba Facebook haikuwajibika vya kutosha na kwamba hilo ni kosa lake binafsi .

Kutokana na hojaji hiyo hisa za mtandao wa Facebook mnamo alasiri siku ya jana ziliongezeka mpaka kufikia asilimia nne , nao Wanasheria nchini Uingereza na Marekani wameanzisha mashtaka dhidi ya Facebook, Cambridge Analytica, na makampuni mengine mawili yanayounganishwa na kesi hiyo

Mark Zuckerberg amejitetea kwa muda wa saa tano katika jopo la wasikilizaji kutoka bunge la seneti la Marekani linalohusika na masuala ya biashara na kamati ya mahakama.

Na baada ya utetezi wake Mark ameeleza hisia zake kutokana na mtandao wa Facebook hapa ulipofikia na yanayojiri hafurahishwi na chochote .

Mark pia hakusita kugusia sintofahamu aliyoiita vita iliyoko baina ya kampuni yake dhidi ya nchi ya Urusi ambayo imefanya majaribio kadhaa kujaribu kutumia data za kampuni yake, majaribio anayoyaona kama vita vya mapambano ya silaha.

Utetezi wa Mark Zuckerberg, umepokelewa vyema na masoko ya hisa na hivyo kuifaidia Facebook kwa ongezeko la hisa asilimia nne unusu.

ADD YOUR COMMENTS

You must be logged in to post a comment Login