Andres Iniesta Aikacha Barcelona.......Anaenda Timu Gani? Soma Hapa - OFFICIAL ROBENGO BLOG
BannerFans.com

MICHEZO

Andres Iniesta Aikacha Barcelona…….Anaenda Timu Gani? Soma Hapa

on

Kiungo mchezeshaji wa klabu ya Soka ya Barcelona, Andres Iniesta (33) ametangaza kuondoka klabuni hapo ifikapo mwisho wa msimu huu 2017/18.

Kiungo huyo raia wa Uhispania aliyeichezea klabu hiyo kwa miaka 22 na kushinda mataji 31 amesema hataweza kucheza dhidi ya Barcelona atakapoondoka klabuni hapo.

Iniesta maarufu kama ‘Magician’ ni mchezaji pekee kuwahi kuwa mchezaji bora (Man of the match) katika fainali ya EUROs, fainali ya Kombe la Dunia na fainali ya Klabu Bingwa Ulaya.

Kiuongo huyo bora duniani anatarajiwa kwenda kukipiga China ambapo inadaiwa atalipwa mkwanja mara mbili ya ule anaolipwa Barcelona. Aidha, Iniesta amesema hataki tena kucheza Soka Bara la Ulaya kwa sababu atakutana katika mechi na timu yake iliyomlea Barcelona jambo ambalo anaona kwake haitakuwa vyema kupambana na mlezi wake.

Lionel Mess amuaga Iniesta kwa kusema haya “Andrés, thank you for all these years of football. It was a privilege to enjoy this sport by your side and spend so many unforgettable moments together. I wish you all the best in this new stage in sports and in your life. You are a phenomenon, inside and outside the court. We will miss you!!!”

Neyar JR naye aliandika haya “Maestro, who honors to be part of his career in Barcelona, ​​already admired you from afar and after I came to be closer I fell in love with his football and more for the person that you are out of the field … I will always tell the my friends, children and family that I had the pleasure of celebrating goals and titles at his side.
Barcelona thanks you, I thank you and soccer lovers thank you for everything you did !!! Lots of luck on your walk always, hug CAPI !! @ andresiniesta8”

ADD YOUR COMMENTS

You must be logged in to post a comment Login