BURUDANI

Jacqueline Wolper Amchokoza Mzungu wa Harmonize Sara!

on

MKALI wa Bongo Movies, Jacqueline Wolper Massawe na mzungu ambaye ni mpenzi wa Staa wa Bongo fleva kutoka WCB Harmonize, Sarah wamerudi kwenye ya vita ya mtandaoni.

Wolper na Sarah wamerushiana maneno Kwenye mtandao wa Instagram ambapo Sarah amemtuhumu Wolper kwa kumtumia meseji za Siri Harmonize huku akijua wazi kabisa ni mpenzi wake.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Sarah ameandika maneno haya kumtolea povu Wolper na kumchana kuwa anamtongoza Harmonize na kumtumia meseji huku anaona wazi kuwa hamjibu na amemtaka Wolper aishi maisha yake.

Hii sio mara ya kwanza kwa Wolper na Sarah kugombana kisa penzi la Harmonize, siku za nyuma Sarah ameshawahi kuanika kuwa Wolper bado anamtaka Harmonize jambo ambalo Wolper amekuwa akikataa siku zote.

ADD YOUR COMMENTS

You must be logged in to post a comment Login