MICHEZO

Baada Ya Kufunga Hat-Trick Mchezaji Lionel Messi Apata Dili Hili Hapa!

on

Mshambuliaji wa klabu ya Barcelona, Lionel Messi amesaini dili nono na shirika la ‘World Tourism Organisation’ (UNWTO) linalojishughulisha na masuala  ya utalii ambalo linafanya kazi chini ya Umoja wa Mataifa.

Kwa mujibu wa mtandao wa klabu hiyo {www.fcbarcelona.com} Messi amesaini dili hilo Jumamosi iliyopita baada ya mchezo wa La Liga kati ya FC Barcelona na Leganes kwenye mchezo ambao Messi alitupia magoli matatu.

Katibu Mkuu wa UNWTO, Zurab Pololokashvili wakati akimtambulisha Messi leo Aprili 09, 2018 amesema kuwa ni heshima kubwa kwa shirika hilo kufanya kazi na Messi.

“Messi ni moja ya wachezaji wakubwa duniani ni heshima kwa shirika letu kufanya naye tunajua ni mtu mwenye mitazamo chanya na anajituma sana uwanjani, bila shaka hii heshima kwetu,“alisema Zurab Pololokashvili.

Kwa upande wake Messi yeye amesema ni mafanikio makubwa kufanya kazi na shirika hilo na anaamini kuwa atafanya nao kazi vizuri kutangaza utalii.

Messi ameungana na mastaa wengine kama Fernando Hierro na kocha wa zamani wa Real Madrid na timu ya Hispania, Vicente del Bosque.

ADD YOUR COMMENTS

You must be logged in to post a comment Login