BIASHARA

TFDA yazindua mafunzo ya siku 2 ya wasindikaji wadogo wa vyakula wilayani Mbozi.

on

Mamlaka ya chakula na dawa TFDA hapo jana imetoa mafunzo kwa wajasiliamali wadogo wa usindikaji wa vyakula yatakayofanyika  kwa siku 2 kuanzia leo tarehe 20/03/2018 hadi tarehe 21/03/2018 katika ukumbi wa mkolla holl uliopo vwawa wilayani Mbozi kwaajili ya kuviwezesha vikundi hivyo kufanya ujasiliamali wenye tija na kuboresha bidhaa ili kuweza kukuidhi viwango vya ushindani katika soko la ndani na nje.

Akiwasilisha taarifa kwa mgeni rasmi mganga mkuu wa mkoa wa Songwe alisem kutokana na tathimini iliyofanyika mwaka 2006 na 2097 ilionyesha kwamba 74% ya viwanda ni viwanda vidogo na ndiomaana wao wanachukua jukumu la kuhakikisha mafunzo yanafanyika kwa wasindikaji wadogo wa vyakula.

Amesema pamoja na mchanganuo huo kumekuwa na changamoto nyingi kwa wasindikaji wadogo wa vyakula kutokidhi matakwa ya sheria ya chakula, dawa na vipodozi na changamoto zingine kama majengo kukosa sifa na wajasiliamali wengi kutosajili bidhaa zao kutokana na kushindwa kumudu ghalama za usajili wa bidhaa.

Baadhi ya wajasiliamali walio hudhulia katika mafunzo hayo akiwemo Ruth Enjewele wameiomba mamlaka hiyo  iweze kuwasaidia maeneo maalumu ya kufanyia usindikaji na mitaji ili kuweza kumudu mahitaji kama kupata vitendea kazi bora zaaidi, wakati Peter Mwansite aliweza kuiomba mamlaka hiyo kusaidia upatikanaji wa vifungashio bora zaidi ili waweze kukidhi soko la ushindani ndani na nje ya nchi

Kaimu mkurugenzi wa TFDA Lusajo Mwalukasa amesema mamlaka ya chakula na dawa inatoa mafunzo hayo baada ya  kufanya ukaguzi wa bidhaa mbalimbali zinazosindikwa na viwanda hivyo na kutambua kuwa bidhaa zote zinamapungufu mengi ikiwemo kukosa ukaguzi na nembo za TFDA na TBS hivyo kukosa sifa katika soko la ushindani.

Amesema hii ni fulsa nzuri kwa wajasiliamali kuweza kujifunza na kupata mwanga juu ya changato zinazo wakabili kuweza kufanya ujasiliamali wenye tija na unaofuata vigezo ili bidhaa ziweze kukubalika  na hivyo kufanya  vikundi kuweza kusonga mbele zaidi na kuinua uchumi wa viwanda hapa nchini na hivyo kulisadia taifa kuweza kufikia malengo ya nchi ya uchumi wa kati ifikapo 2025.

 

 

ADD YOUR COMMENTS

You must be logged in to post a comment Login