Man City na Juventus Zatinga Robo fainali michuano ya UEFA Champions League - OFFICIAL ROBENGO BLOG
BannerFans.com

MICHEZO

Man City na Juventus Zatinga Robo fainali michuano ya UEFA Champions League

on

Siku moja baada ya kuzishuhudia timu za Real Madrid na Liverpool zikitinga hatua ya robo fainali ya michuano ya UEFA Champions League msimu wa 2017/2018, jana tumeshuhudia timu nyingine mbili zikifanikiwa kuungana na Real Madrid na Liverpool katika hatua ya robo fainali na sasa wanasubiri droo.

Club za Man City na Juventus leo zimefanikiwa kutinga hatua ya robo fainali ya michuano ya UEFA Champions League, Man City licha ya kupoteza nyumbani kwa magoli 2-1 dhidi ya FC Basel leo, wamefanikiwa kuingia robo fainali kwa kuwa na aggregate ya magoli ushindi wa magoli 5-2, hiyo ni baada ya kufanikiwa kuvuna ushindi wa magoli 4-0 katika mchezo wa kwanza ugenini.

Kwa upande wa Juventus shukrani pekee zimuendele Paulo Dybala aliyefunga goli la ushindi dakika ya 67 lililoinusuru Juventus kuaga michuano ya Champions League kama game ingemalizika kwa sare ya kufungana goli 1-1 katika uwanja wa Wembley.

Mchezo wa kwanza nchini Italia ulimalizika kwa Tottenham na Juventus kufungana kwa sare ya magoli 2-2, hivyo ushindi wa Juventus wa 2-1 unaipeleka Juventus robo fainali kwa kupita kwa jumla ya aggregate ya magoli 3-4.

Mashabiki wa Juventus ya Italia waliyosafiri kutoka Italia hadi London wakiwa wameshikilia mabango ya kumkumbuka nahodha wa Fiorentino Davide Astori aliyefariki akiwa amelala hotelini.

ADD YOUR COMMENTS

You must be logged in to post a comment Login