MICHEZO

FA yamuadhibu Pep Guardola na kumpa Onyo Kali…..Sababu Ni Hii hapa!

on

Chama cha soka England FA leo Ijumaa ya March 9 2018 kimetangaza maamuzi yake kuhusiana na kocha wa Man City raia wa Hispania Pep Guardiola ambaye aliingia kwenyea headlines kwa kuvaa ribbon ya njano katika game za EPL.

FA walimpa muda wa kujitetea Pep Guardiola kutokana na kitendo chake cha kupenda kuvaa ribbon ya njano mara kwa mara katika game za Ligi Kuu England, nembo ambayo inahusishwa na masuala ya kisiasa nchini Hispania.

Hivyo FA leo imetangaza kumpa onyo kali na kumpiga faini ya pound 20,000 (Tsh milioni 62.4) kwa kosa hilo lakini Kama utakuwa unakumbuka vizuri Pep Guardiola amekuwa akivaa nembo hiyo ambayo inatumika na kutafsirika nchini kwao Hispania na watu wanaodai uhuru wa jimbo la Catalunya kujitenga na Hispania.

ADD YOUR COMMENTS

You must be logged in to post a comment Login