BURUDANI

Alichotamka Johnson Nguza ‘Papii Kocha’ Juu ya mwanaye!

on

MWANAMUZIKI mahiri wa Dansi Bongo, Johnson Nguza ‘Papii Kocha’ anaona fahari na ushujaa kila anapomuangalia mtoto wake, Asha ambaye alimuacha akiwa mdogo wakati akitumikia kifungo.

Papii alisema kuwa, alipokuwa gerezani takriban miaka 14, hakupata muda mzuri wa kukaa na mtoto wake huyo zaidi ya alivyokuwa akienda kumsalimia gerezani, lakini kwa sasa ameona afanye kila analoweza mwanaye aweze kufaidi angalau matunda na furaha aliyoikosa kwa muda mrefu kutoka kwake.

“Unajua sijakaa na mtoto wangu kwa kipindi kirefu sana na hivi sasa ndiyo anatakiwa afaidi matunda kutoka kwa baba yake hivyo ni lazima nifanye kazi kwa jasho jingi ili ayafaidi matunda yangu,” alisema Papii.

Hata hivyo, Papii amewaomba mashabiki wake wajitokeze kwa wingi kwenye shoo yao inayotarajiwa kufanyika Machi 10, mwaka huu katika Ukumbi wa King Solomon, Namanga jijini Dar.

ADD YOUR COMMENTS

You must be logged in to post a comment Login