BURUDANI

Tunda Afanya maamuzi Magumu………….Je Aunty Ezekiel Atamjibu nini?

on

Ni miezi kadhaa sasa imekatika tangu video vixen maarufu hapa nchini Tanzania Tunda alirushiana maneno na muigizaji Aunty Ezekiel  pamoja na mzazi mwenzake Mose Iyobo na kusemekana kuwa Tunda alishindwa kulipa deni alilokuwa akidaiwa na Aunty Ezekiel.

Leo March 10,2018 kupitia mtandao wa instagram wa Tunda ameomba radhi kwa kile ambacho alikifanya dhidi ya Aunty na kuamini kuwa hata yeye atakuwa mama wa baadae, hivyo ameamua kumuomba radhi Aunty.

“Let me take this opportunity kumuomba radhi Aunty kwa kumtukana mtoto wake ilikuwa ni hasira naomba msamaha kama mwanamke ambaye nitaitwa mama pia soon” aliandika tunda kupitia ukurasa wake wa Instagram, lakini Ujumbe huo pia umezua maswali kuwa Tunda ni mjamzito? kwa nini asema atakuwa mama soon?.

ADD YOUR COMMENTS