MICHEZO

Manchester United Walaza Liverpool Goli 2 kwa 1 Old Trafford

on

MICHEZO:Jumamosi ya March 10 2018 katika uwanja wa Old Trafford Man United waliikaribisha Liverpool kucheza mchezo wao wa Ligi Kuu England msimu wa 2017/2018, huo ukiwa ni mchezo wa kumaliza ubishi kati ya Jurgen Klopp na Jose Mourinho.

Mchezo huo ambao umechezwa Old Trafford umemalizika kwa Man United kupata ushindi wa magoli 2-1, magoli ya Man United yote yakifungwa na Marcus Rashford dakika ya 14 na 24 wakati goli pekee la Liverpool kilipatikana kwa beki wa Man United Eric Bailly kujifunga dakika ya 66 baada ya kushindwa kuzuia mpira uliopigwa na Sadio Mane. 

Huo unakuwa ni ushindi wa 88 wa Man United dhidi ya Liverpool toka wakutane kwa mara ya kwanza April 28 1894 katika mchezo uliyomalizika kwa Liverpool kushinda kwa magoli 2-0, hadi kufikia leo Man United na Lverpool wamecheza jumla ya game 228, wakitoka sare game 65 huku Liverpool akishinda katika game 75 pekee.

ADD YOUR COMMENTS