BannerFans.com

BURUDANI

Zari Atangaza Rasmi Kuachana na Diamond

on

IKIWA ni siku ya wapendanao,  leo Februari 14, 2018, Mfanyabiashara maarufu Afrika Mashariki, Kati na Kusini, Zarinah Hassan ‘Zari the Boss Lady ametangaza kuvunja rasmi mahusiano yake ya kimapenzi na Staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.

Kupitia ukurasa wake wa Instagaram, Zari amefunguka kuwa kilichompelekea kufanya hivyo ni kutokana na Diamond kutokuwa mwaminifu kwenye mahusiano yao huku akibainisha kuwa kuachana katika mahusiano ya kimapenzi hakutaathiri uhusiano wao kama wazazi.

Diamond ambaye alianza mahusiano na Zari takribani miaka mitano iliyopita baada ya kuachana na staa wa Bongo Movies, Wema Sepetu, amezaa na Zari watoto wawili ambao ni Tiffah na Nilan huku pia akitajwa kuchepuka jambo ambalo limepelekea akazaa mtoto mwingine na mwanamitindo Hamissa Mobeto.

Mbali na Mobeto, Diamond amekuwa akihusishwa kurudiana na Wema ambapo hivi karibuni walionekana kugandana kwenye hafla ya kutambulishwa kwa msanii Mbosso kwenye lebo ya WCB Wasafi.

Bado haijathibitika moja kwa moja iwapo kweli wameachana ama ni kiki kama ambavyo wasanii wengine wamekuwa wakifanya.

Zari ameandika;

Understand that this is very difficult for me to do. There have been multiple rumors some with evidence floating around in ALL SORTS of media in regards to Diamond’s constant cheating and sadly I have decided to end my relationship with Diamond, as my RESPECT, INTEGRITY, DIGNITY & WELL BEING cannot be compromised. We are separating as partners but not as parents. This doesn’t reduce me as a self-made individual, and as a caring mother, and the boss lady you have all come to know. I will continue to build as a mogul, i will inspire the world of women to become boss ladies too. I will teach my four sons to always respect women, and teach my daughter what self-respect means. Unlike many, I’ve been in the entertainment industry for 12 years, and through all my challenges I came out a victor because I am a winner, and so are all of you Zari supporters.
HAPPY VALENTINE’S.

ADD YOUR COMMENTS

You must be logged in to post a comment Login