MTANDAONI

Mwanaume amebeba cocaine kwenye makalio bandia ashikwa Ureno

on

Polisi nchini Ureno wamemkamata mwanamume mmoja kwenye uwanja wa ndege huko Lisbon, ambaye alikuwa amebeba kilo moja ya cocaine kwenye makalio bandia.

Vyombo vya habari nchini humo vilisema kuwa raia huyo wa Brazil aliwasili kwa ndege kutoka mji wa Belém do Pará, kaskazini mwa Brazil.

Haijulikani ni vipi polisi walifanikiwa kugundia hilo

Mwanamume mwingine ambaye anashukiwa kuwa angepokea dawa hizo alikamatwa kwenye kituo cha treni cha mji huo.

Wanaume hao watakabiliwa na kesi ya ulanguzi wa madawa ya kulevya.

  • http://robengo16.com/2017/09/rais-wa-ufilipino-akubali-mwanae-auawe-kisa-madawa-ya-kulevya/

ADD YOUR COMMENTS

You must be logged in to post a comment Login