KITAIFA

Mualiko Wa Kim Jong-un Ulivyo Jazwa Masharti Na Korea Kusini

on

Waziri mkuu wa Korea kusini Lee Nak-yeon amebaini wazi kwamba kuna masharti ambayo lazima yabainishwe kabla ya kukubali mwaliko wa uongozi wa nchi hiyo kukutana na kiongozi wa Korea kaskazini, Kim Jong-un.

Jana katika hatua kubwa ya kidiplomasia kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un, alimwalika mwenzake wa kusini kwa mkutano lakini Rais Moon Jae-in bado hajatoa jibu la kuitikia wito huo au la.

Ujumbe huo umetolewa na dada yake kiongozi wa Korea kaskazini Kim Jong un ambaye aliandamana na maafisa wa ngazi za juu zaidi wa Korea Kaskazini kuwahi kuzuru Korea Kusini tangu kumalizika kwa vita vya Korea miaka 60 iliyopita.

Hata hivyo hatua hiyo haijafurahiwa na Marekani ambayo ingali inataka kwanza Korea kaskazini ishinikizwe kuachana na miradi yake ya nyuklia.

ADD YOUR COMMENTS

You must be logged in to post a comment Login