KITAIFA

Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti Amelivunja Baraza La Ardhi

on

Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti amelivunja baraza la ardhi la Kata ya Murray wilayani Mbulu mkoani Manyara baada ya wananchi kulalamika kunyanyaswa, kuombwa rushwa na kunyimwa haki zao. Akizungumza jana Februari 12, 2018 baada ya kulivunja baraza hilo, Mnyeti amesema hawezi kuliacha liendelee kufanya kazi kwenye eneo hilo wakati wananchi wanalalamikia kukosa haki zao.

Amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya mji wa Mbulu, Anna Mbogo kuanza mchakato wa kupatikana viongozi wapya, waadilifu wa baraza la kata hiyo ili waendelee kuwatumikia wananchi. Amesema mikutano ya wananchi kuwachagua wajumbe wengine inatakiwa kuanza upya ili nafasi za wajumbe wapya zipatikane na kuhudumia jamii ya eneo hilo.

“Tafuteni watu waadilifu, wenye weledi na hofu ya Mungu ambao wanaweza kuwahudumia wananchi ili washike nafasi hizo na kutekeleza majukumu yao ipasavyo,” amesema Mnyeti. Amesema kuwa baada ya kuwaondoa viongozi wa baraza hilo linalodaiwa kupokea rushwa.

ADD YOUR COMMENTS

You must be logged in to post a comment Login