BannerFans.com

KIMATAIFA

Kiongozi Wa NRM ‘Miguna’ Asafirishwa Kwa Nguvu Kuelekea Canada

on

Mwanasiasa wa muungano wa upinzani nchin Kenya Nasa, Miguna Miguna amefurushwa na kupelekwa nchini Canada kupitia ndege ya KLM , kwa mujibu wa wakili wake Nelson Havi na Cliff Ombeta.

Bwana Ombeta amesema kuwa aliarifiwa kwamba bwana Miguna aliingizwa katika ndege iliokuwa ikielekea Amsterdam na baadaye kuelekea Canada.

Wakili mwengine Dkt. John Khaminwa alisema kuwa mteja wake tayari ameondoka Kenya.

“Ni kweli .Alilazimishwa kuingia katika ndege ya KLM dakika chache tu kabla ya saa nne usiku na tumebaini kwamba anaelekea Canada. Ni ukiukaji mkubwa wa haki”, alisema Dkt Khaminwa kwa simu.

Haijulikani ni sheria gani iliotumiwa na serikali kumuondoa nchini Kenya kwa kuwa katiba inampatia haki kama raia wa Kenya kwa kuwa ni mzaliwa wa taifa hilo.

Anasema kwamba wakati Miguna alipokamatwa , serikali ya Canada ilikuwa imeiandikia Kenya kionyesha wasiwasi kwamba raia wake alikuwa ananyanyaswa na walitaka arudishwe nchini humo.

Bwana Miguna siku ya Jumanne alielezea vile alivyokamatwa bila mawasiliano na familia yake ama wakili wake kwa siku tano.

Alisema kuwa maafisa wa polisi walimnyanyasa kwa kumfungia katika maeneo ambayo hayafai kwa binaadamu.

Bwana Miguna alikuwa akizungumza katika mahakama ya kajiado ambapo alipelekwa baada ya kukamatwa kwake siku ya Ijumaa kwa tuhuma za kushiriki katika sherehe ya kumuapisha kiongozi wa upinzani Raila Odinga ambaye aliapishwa kuwa rais wa wawananchi tarehe 30 Januari.

Ripoti za kufurushwa nchini Kenya zilijiri saa chache baada ya jaji wa mahakama kuu Luka Kimaru kumzuia mkurugenzi wa Ujasusi na inspekta jenerali wa polisi dhidi ya kumwekea mashtaka yoyote.

ADD YOUR COMMENTS

You must be logged in to post a comment Login