BannerFans.com

MICHEZO

Kelvin yondan Awaacha Yanga Midomo Wazi, Yanga Haawatakuja Kumsahau!

on

Kelvin Yondani, juzi Jumamosi alifanya jambo ambalo liliwaacha vinywa wazi wapenzi na mashabiki wa timu hiyo katika mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Lipuli FC kwenye Uwanja wa Samora, Iringa.

Katika mchezo ambao Yanga ilishinda mabao 2-0, Yondani hakutakiwa kucheza kutokana na kuwa mgonjwa kama ilivyokuwa kwa Andrew Vincent ‘Dante’.

Waliotakiwa kuiongoza safu ya ulinzi ya Yanga katika mechi hiyo ni Juma Makapu na Maka Edward, lakini baada ya Yondani kuona hivyo aliamua kuji­toa na kumwambia kocha wake mkuu, Mzambia, George Lwandamina kuwa itabidi acheze kwa ajili ya kuisaidia timu yake ili iweze kupata ushindi.

Akizungumza na Championi Jumatatu, mmoja wa viongozi wa benchi la ufundi la Yanga ambaye aliomba kuto­tajwa jina lake akihofia kuchukuliwa hatua kwa sababu ametoa siri ya timu kinyume na taratibu, alisema kuwa mwanzoni Lwandamina alikataa Yondani asicheze lakini baada ya kushauriana na wenzake aliamua kump­anga.

“Hakika jamaa ame­onyesha kuwa ni mche­zaji wa aina gani ambaye yupo tayari kuhatarisha maisha yake kwa sababu ya timu,“Kwa kiwango ali­choonyesha katika mechi hii licha ya kuwa anaumwa, alimshangaza pia Lwandamina,” alisema kiongozi huyo.

Alipoulizwa Yondani kuhusiana na hilo hakuwa tayari kusema chochote lakini Lwandamina alisema kuwa anam­pongeza kwa kazi nzuri aliyoifanya katika mechi hiyo japokuwa hakuwa fiti kwa asilimia miamoja.

ADD YOUR COMMENTS

You must be logged in to post a comment Login