SIASA

Chadema Wapata Pigo Lingine Wilayani Mbulu Mkoani Manyara

on

Diwani wa Kata ya Hayderer (Chadema) wilayani Mbulu mkoani Manyara, Justin Masuja amejiuzulu nafasi hiyo na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) jana Februari 12,2018 katika ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti.

Katika mkutano wa hadhara, Mnyeti aliwaomba madiwani wa upinzani kuhamia chama tawala ili watekeleze Ilani ya CCM ambayo ndiyo ipo madarakani.

Masuja alieleza kwamba amejiunga na CCM ikiwa ni hatua ya kuunga mkono jitihada za Rais John Magufuli katika kuwatumikia wananchi wa Tanzania.

ADD YOUR COMMENTS

You must be logged in to post a comment Login