Watu 36 Wapoteza Maisha Katika Ajali Ya Basi Nchini Peru - OFFICIAL ROBENGO BLOG
BannerFans.com

KIMATAIFA

Watu 36 Wapoteza Maisha Katika Ajali Ya Basi Nchini Peru

on

Takriban watu 36 wameuawa baada ya basi kupingirika mita 100 chini ya mteremko na kuanguka kwenye fukwe nchini Peru.

Wizara ya afya ilisema kwa manusura sita hadi saa wameondolewa kutoka kwa mabaki ya basi hilo na kupelekwa hospitalini. Ajali hiyo ilitokea katika eneo linalofahamika kwa ajali nyingi linalofahamika pia kama (kona ya shetani) eneo la Pasamayo kaskazini mwa mji mkuu Lima.

Afisa mmoja alisema kuwa basi hilo lilikuwa limebeba takriban watu 50. Babarara hiyo iliyo kando mwa habari ya Pacific inatajwa kuwa moja ya zile hatari zaidi nchini Peru.Rais wa Peru Pedro Pablo Kuczynski, alisma kuwa ni jambo la kusikitisha na uchungu mwingi ikiwa nchi itakumbwa na ajali kama hiyo.

Alitumia ujumbe wa rambi rambi kwa familia za waathiriwa. Picha kutoka eneo hilo zilionyesha waokoaji wakizunguka mabaki ya basi hilo huku watu wakitazama kutoka juu.

ADD YOUR COMMENTS

You must be logged in to post a comment Login