Utolewaji Wa Chakula Mashuleni Kumeongeza Ufaulu Kwa Wanafunzi Mkoani Songwe - OFFICIAL ROBENGO BLOG
BannerFans.com

ELIMU

Utolewaji Wa Chakula Mashuleni Kumeongeza Ufaulu Kwa Wanafunzi Mkoani Songwe

on

Imebainika kuwa utolewaji wa chakula kwa wananfunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mbozi mkoani Songwe kumepunguza utoro na kuongeza kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi wa darasa la saba na kidato cha piili katika matokeo ya mwaka 2017 .

Hayo yamebainishwa na maofisa elimu msingi na sekondari wilayani Mbozi mkoani hapa Hossana Nshullo na Sophia Shitindi mbele ya baraza la madiwani kuwa kufuatia utekelezaji wa agizo la kamati ya fedha la kila shule kutoa chakula cha mchana kwa wanafunzi utoro umepungua klwa kiwango kikubwa kwa shule za msingi na msingi hali iliyochangia ongezeko la wanafunzi waliofaulu kujiunga kidato cha kwanza.

Diwani wa kata ya Ipunga Barton Sinyenga amesema kuwa kwa kuwa matokeo ya utafiti uliofanyika ulibaini kuwa utolewaji wa chakula shuleni unaongeza ufaulu kwa wanafunzi hivyo wao kama baraza waliona kuwa utafiti huo unaweza kuwasaidia na matokeo yameanza kupatikana kwa kiwango cha ufaulu kuongezeka na kuwataka wazazi kuunga mkono mpango huo ili kukuza kiwango cha elimu.

Naye Maarifa Mwashitete diwani wa kata ya Halungu amesema kuwa zoezi hilo limeleta mafanikio makubwa katika kata yake ukilinganisha na kipindi ambacho chakula kilikuwa hakitolewi hivyo ni vigumu kusitisha utioaji wa chakula kwa kuwa watakaoathirika ni watoto ambao huanza shule wakiwa wadogo chini ya miaka 6 hivyo wanashindwa kusoma wakiwa na njaa na chakula ni suluhisho pekee lililoonekana kuwa kichocheo cha matokeo chanya.

Kwa upande wake mwenyekiti wa halimashauri ya wilaya ya Mbozi Erick Ambakisye amesema kuwa wao kama serikali za mitaa hawapingani na tamko la raisi bali wanaliunga mkono kwa asilimia 100% lakini ili kutimiza adhima yao kama halimashauri ya kutoa chakula kila shule kwa msimu huu imetenga ekari nne za mahindi kwa ajili ya kuzalisha chakula cha wanafunzi ili kuwapunguzia mzigo wazazi na kuziagiza shule kuzalisha chakula katika maeneo yao.

Aidha Minga amesema kuwa hawatoruhusu mwanafunzi yeyote kurudishwa nyumbani kwasababu ya kutochangia chakula shuleni kwani awamu ya kwanza wazazi walitoa michango yao kulingana na idadi ya wanafunzi hali iliyochangia ongezeko la ufaulu kwa darasa la saba na kusababisha uhaba wa vyumba vya madarasa zaidi ya 60n kwa shule za sekondari na kuwaagiza watendaji wote ambao hawajakamilisha ujenzi wa vyumba vya madarasa kukamilisha haraka iwezekanavyo.

ADD YOUR COMMENTS

You must be logged in to post a comment Login