Utani Wa Mhe. Paul Makonda Kwa Mhe. Mbowe - OFFICIAL ROBENGO BLOG
BannerFans.com

MTANDAONI

Utani Wa Mhe. Paul Makonda Kwa Mhe. Mbowe

on

Leo January 9 tumeshuhudia Mhe Edward Lowassa akienda ikulu kumwagia sifa rais John Pombe Magufuli suala ambalo limezua utata na mshangao kwa watu wengi juu ya jambo hilo, kwani mhe. Lowassa ni kiongozi wa upinzni.

Mhe. Edward Lowassa leo alikwenda ikulu kama moja ya ziara yake lakini kitendo hicho kimezua mshangao mkubwa kwa baina ya watu na wanachama wa CHADEMA kwani wao kama upinzani kupitia msemaji wao Freeman Mboye amedai kwamba hakuna jema analolifanya Rais Magufuli.

Lakini si huyo tu kutoka upinzani aliyetoa tamko mara baada ya Lowassa kumwagia sifa Rais Magufuli bali Lema naye alitoa kauli za kutokukubaliana na kauli za Lowassa alipokuwa Ikulu.

Lakini Mhe Paul Makonda amepost Picha ya huzuni ya Mbowe na kuandika ujumbe huu “Kaka yangu mpendwa anawatakia usiku mwema.” suala ambalo pia limezua minong`ono na comment nyingi katika post hiyo ya Makonda.

ADD YOUR COMMENTS

You must be logged in to post a comment Login