Takribani Watu 13 Wamefariki Katika Maporomoko Ya Maji Calfonia Marekani - OFFICIAL ROBENGO BLOG
BannerFans.com

KIMATAIFA

Takribani Watu 13 Wamefariki Katika Maporomoko Ya Maji Calfonia Marekani

on

Watu 13 wamefariki kutokana na maporomoko ya ardhi yaliyosababishwa na mvua kubwa kusini mwa jimbo la California, Marekani, maafisa wamesema. Wengine 163 wamelazwa hospitali, 20 wakiwa na majeraha yanayohusiana na mvua kubwa.Wanne wana majeraha mabaya.

Watu wapatao 300 wanadaiwa kukwamba katika hori ya Romero, mashariki mwa mji wa Santa Barbara. Polisi wamesema eneo lililokumbwa na maporomoko hayo linafanana na “uwanja wa vita wakati wa Vita Vikuu vya Kwanza vya Dunia”.

Mafuriko na maporomoko ya ardhi yameathiri baadhi ya maeneo ambayo yaliathiriwa na moto mkubwa wa nyika na yameharibu barabara kuu ya pwani umbali wa maili 30 (48km). Maafisa wa uokoaji wamesema kuna watu kadha ambao hawajulikani waliko na kwamba idadi ya waliofariki inatarajiwa kupanda.

Maafisa wa Kikosi cha Ulinzi Baharini wametuma ndege kadha kusaidia juhudi za uokoaji na wametahadharisha umma dhidi ya kutumia ndege zisizo na marubani kwani zitatatiza juhudi za uokoaji.

Maelfu ya wakazi wa California waliamrishwa kuondoka makwao Jumatatu, mara ya pili katika kipindi cha miezi miwili. Mara ya kwanza ilikuwa ni kwa sababu ya moto, wakati huu ni kwa sababu ya mvua.

ADD YOUR COMMENTS

You must be logged in to post a comment Login