Rais Magufuli ametangaza uamuzi huo katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu Jijini DSM ya kumuapisha Dotto Biteko kuwa Naibu Waziri wa Madini. Ambapo amemteua Prof. Shukuruni Elisha Manya kuwa Kamishina wa Madini.

“Nimeambiwa Kamishina wa Madini ni tatizo inawezekana yupo hapa, Nimeamua kumteua Prof. Elisha Manya atakuwa Kamishina wa Madini na ndo atakuwa Mtendaji Mkuu wa Tume ya Madini.”– Amesema Rais Magufuli.

Aidha ameeleza kuwa baadhi ya watendaji anaowateua bado hawajaelewa anataka nini, na kusema kuwa hafahamu wizara ya madini ina matatizo gani.

Hivyo amewata viongozi wanaoteuliwa kufanya kazi ili kuwaamsha viongozi waliolala serikalini.