Nandy Atamani Kuwa Mwandani wa Mwanamuziki Wa Rapp BillNas - OFFICIAL ROBENGO BLOG
BannerFans.com

BURUDANI

Nandy Atamani Kuwa Mwandani wa Mwanamuziki Wa Rapp BillNas

on

Binti anayefanya vizuri kwenye Bongo-fleva, Faustina Charles ‘Nandy’ amefunguka kuwa kama kutoa penzi ni bora kwa mwanamuziki mwenzake, Billnas na sio Dogo Janja kama wanavyosema watu.

Nandi alikanusha kwa kusema kuwa watu wengi wanasema kuwa wimbo alioimba wa Kivuruge amemuimbia Dogo Janja baada ya kumtema.

“Sijawahi kuwa na uhusiano na Dogo Janja ila ni mshikaji tu na sijamfikiria labda mngeniambia Billnas ni mtu ambaye ninampenda na ninatamani siku moja awe wangu ila kama atanifuata yeye,” alisema Nandy.

ADD YOUR COMMENTS

You must be logged in to post a comment Login