Mourinho Huenda Akatimka Na Kuicha Manchester Solemba - OFFICIAL ROBENGO BLOG
BannerFans.com

MICHEZO

Mourinho Huenda Akatimka Na Kuicha Manchester Solemba

on

Kumekuwa na wasiwasi ndani ya klabu ya Manchester United kuwa huenda meneja wa timu hiyo, Jose Mourhno akaondoka Old Trafford msimu ujao.

Meneja wa Manchester United, Jose Mourinho akiwasili Lowry Hotel jana jioni siku ya Jumatano

Kumeanza kuwa na minong’ono ya chini kwa chini kutoka ndani ya United kuwa zimeanza kuonekana dalili za awali zinazoonyesha Mourinho huenda akavunja mkataba wake mwishoni mwa msimu.

Wafanyakazi ndani ya United wanamuona Mourinho akifundisha timu hiyo akiwa mwenyewe huku akitumia muda mchache zaidi kuliko kawaida ya Manchester.

Inaaminika kuwa Jose Mourinho alitumia ndege binafsi wakati wa sikukuu ya Christmas hali isyo kuwa ya kawaida huku akifundisha wachezaji wake tarehe 24 asubuhi na 25 jioni kabla ya kuwapatia mapumziko ya siku chache.

Taarifa kutoka ndani ya klabu zinasema kuwa hawafahamu juu ya ndege hiyo binafsi inayozungumzwa ambayo Mourinho ameitumia kwa matumizi binafsi.  

ADD YOUR COMMENTS

You must be logged in to post a comment Login