Meli Yenye Bendera Ya Tanzania Yakamatwa Ikiwa Na Siraha Ikielekea Nchini Libya - OFFICIAL ROBENGO BLOG
BannerFans.com

KITAIFA

Meli Yenye Bendera Ya Tanzania Yakamatwa Ikiwa Na Siraha Ikielekea Nchini Libya

on

Jeshi la Majini nchini Ugiriki limeishikilia meli yenye bendera ya Tanzania ambayo imebeba vilipuzi ikielekea nchini Libya.

Meli hiyo inadaiwa kusafirisha vilipuzi hivyo kutoka Uturuki kwenda Libya kinyume na marufuku iliyowekwa ya kutosafirisha silaha kwenda Libya.

Kwa mujibu wa Mtandao wa BBC Maafisa wanasema meli hiyo ilikuwa imebeba kreti 29 zilizojaa vilipuzi pamoja na kemikali zinazotumiwa kuunda vilipuzi.

Wizara ya Usafiri wa Majini nchini humo kupitia shirika la habari la Ugiriki la ANA imesema meli hiyo ilisimamishwa ikiwa katika kisiwa cha Crete kusini mwa Ugiriki wikiendi iliyopita baada ya kutiliwa shaka na Jeshi la Usalama la Majini.

ADD YOUR COMMENTS

You must be logged in to post a comment Login