Majanga Gani Yamemfika Future? - OFFICIAL ROBENGO BLOG
BannerFans.com

BURUDANI

Majanga Gani Yamemfika Future?

on

Manamuziki wa Marekani Nayvadius DeMun Wilburn ila awapo on the stage anajulikana kama Future, ameamua kufuta post zake zote katika mtandao wa kijamii wa Instagram.Future mwenye tuzo kibao za muziki amefuta kila kitu katika mtandao huo ambao ana watu milioni 11.9 wanaomfuatilia.

Kufuatia hatua hiyo mkali huyo wa muziki kutoka Marekani amewaacha wadau na mashabiki zake katika hali ya sinto fahamu , licha ya kuwa hii imegeuka kuwa kama desturi kwa wasanii na watu maarufu kufuta post zao na kuanza upya huku wengine wakitumia nafasi hiyo kama kuwapa watu attention ya jambo Fulani.

Mwaka 2017 mkali wa RnB,Bongo Ben Pol alifuta post zake zote katika mtandao huo huo na kuanza kuweka picha iliyozua utata huku wengine wakimpa majina tofauti. Hata hivyo Ben alikuwa kiweka watu katika utayari wa kuachia ngoma yake ya ‘Tatu’,lakini pia mwaka huu mwanadada Wema Sepet naye alifuta post zake zote katika ukurasa wake na kuanza upya.

ADD YOUR COMMENTS

You must be logged in to post a comment Login