Kauli Ya Philippe Coutinho Ni Maumivu Kwa Klabu Ya Liverpool - OFFICIAL ROBENGO BLOG
BannerFans.com

MICHEZO

Kauli Ya Philippe Coutinho Ni Maumivu Kwa Klabu Ya Liverpool

on

Kunako soka la kimataifa leohii nakusogezea taarifa inayomuhusu Staa na kiungo mbrazil Philippe Coutinho amesema kuwa sasa uhamisho wake kwenda Barcelona ni ndoto iliyokamilika.

“Mashabiki wa Barcelona tayari nipo hapa, ndoto zimekuwa kweli natumani tunaonana kesho, “ alisema Coutinho kupitia video fupi aliyoiweka katika mtandao wa Twitter.Kumbukizi ya picha Surelez na Coutinho wakiwa pamoja Liverpoll

Kiungo huyo alieleza hisia zake za kutimiza ndoto yake alipokuwa akipigwa picha katika uwanja wa Nou Camp wakati klabu yake mpya ilipokuwa ikicheza na Levante.

Coutinho anatarajiwa kutambulishwa leo kuwa mchezaji mpya wa Barcelona baada ya klabu yake ya Liverpool kukubali kuuza kiungo huyo kwa dau la pauni milioni 142.

Nyota huyu atasaini mkataba wa miaka mitano na klabu itayotaka kumnunu mchezaji huyo italazimika kutoa kiasi cha pauni milioni 355.

ADD YOUR COMMENTS

You must be logged in to post a comment Login