Israel Yatimua Wahamiaji Kutoka Bara Afrika Katika Ardhi Yake - OFFICIAL ROBENGO BLOG
BannerFans.com

KIMATAIFA

Israel Yatimua Wahamiaji Kutoka Bara Afrika Katika Ardhi Yake

on

Serikali ya Israel  yafahamisha kuwa inataraji kuanza zoezi la kuwafukuza wahamiaji haramu kutoka barani Afrika katika ardhi yake au kuwaweka gerezani.Takriban wahamiaji haramu 40 000 kutoka barani Afrika wapo Israel.

Wengi miongoni mwa wahamiji hao wanatoka nchini Erythrea na Sudan.Israel  imewatahadharisha wahamiaji kuondaka Israel katika kipindi cha miezi mitatu laa sivyo watakamtwa na kutupwa gerezani.

Wahamiaji hao  wameombwa kurejea katika mataifa yao au kwenda nchini Rwanda na Uganda.Zoezi la kuwafukuza wahamiaji ambao wamekataliwa maombi yao ya hifadhi Israel limeanza Januari mosi.Israel ilisaini mkataba na Uganda na Rwanda  kuhusu  mapokezi ya wahamiaji hao.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na Haaretz, Israel italipa kiwango cha dola 5000 kwa Rwanda kwa kila mhamiaji mmoja atakaepokelewa nchini humo.Wahamiaji ambao wataondoka Israel kwa hiyari yao kila mmoja atapewa dola 3 500.

ADD YOUR COMMENTS

You must be logged in to post a comment Login